• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshikamano, ushirikiano na uratibu ndio silaha ya binadamu kukabiliana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 17:44:36

    Rais Xi Jinping wa China amesema hivi sasa jumuiya ya kimataifa inahitaji zaidi imani thabiti, ushirikiano na mshikamano, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kujumuisha nguvu za pamoja, na kushirikiana kupata ushindi katika vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona. Rais Xi amesema hayo katika mkutano maalum wa viongozi wa Kundi la Nchi 20 (G20) uliofanyika jana kwa njia ya video.

    Katika kipindi hiki muhimu cha mapambano dhidi ya virusi vya Corona, viongozi wa nchi zenye nguvu zaidi ya kiuchumi na mashirika ya kimataifa wanajadiliana kwa njia ya video, wakiwa na lengo dhahiri la kuratibu sera na vitendo, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na maambukizi, na kutuliza uchumi wa dunia.

    Rais Xi Jinping wa China ametoa ufafanuzi kuhusu uzoefu na ufanisi wa China katika mapambano hayo, na kutoa mapendekezo manne: kushikilia kupiga vita dhidi ya virusi vya Corona duniani, kufanya ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia kuenea kwa virusi, kuunga mkono kazi ya mashirika ya kimataifa, na kuimarisha uratibu wa sera za kiuchumi za nchi mbalimbali. Mapendekezo hayo yameonyesha kuwa "mshikamano, ushirikiano na uratibu", ni utekelezaji halisi wa China wa kusukuma mbele wazo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Jambo lingine muhimu ni kwamba maambukizi yanaharibu uchumi wa nchi wanachama wa G20 na dunia. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva ameonya kuwa, uchumi wa dunia kwa mwaka huu utakuwa na ukuaji hasi, kiasi ambacho kitakuwa kibaya zaidi kuliko mwaka 2008 msukosuko wa kifedha ulipotokea.

    Hivyo rais Xi ametoa wito kwa nchi mbalimbali kuongeza nguvu za kusaidiana kwa sera zao za kiuchumi, kuchukua hatua za pamoja, kupunguza na kusamehe ushuru, kuondoa vikwazo, kurahisisha biashara, na kulinda kwa pamoja utulivu wa mnyororo wa uzalishaji na utoaji wa dunia, ili kuzuia uchumi wa dunia kudidimia. Pia amesema, China itaendelea kufungua mlango na kufanya mageuzi, kupanua kigezo cha kuingia katika soko la China, kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara, pia kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na uwekezaji katika nchi za nje. Hii ni ahadi muhimu ya China kwa ajili ya kutuliza uchumi wa dunia, pia ni majukumu yake ikiwa nchi kubwa.

    Mwenyekiti wa klabu ya kampuni 48 ya Uingereza Stephen Perry amesema, China inatumia kitendo chake kuonyesha umuhimu wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, msimamo huo wa ushirikiano na wazi unaostahili kuigwa na nchi mbalimbali katika kukabiliana na masuala ya kimataifa katika siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako