• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar: SMZ kutathmini uchumi baada ya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-30 16:56:11
    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), inakusudia kutathmini hali ya uchumi katika miradi yake na utalii kutokana na tishio la ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

    Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia, alisema hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na SMZ.

    Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa nyumba za maendeleo ya makazi ya wananchiKwahani mkoa wa mjini, magharibi Unguja, na ujenzi wa jengo la mahakama kuu ya Zanzibar Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja.

    Amesema serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kumalizika kwa wakati licha ya kuwepo hofu ya coronana uhaba wa mchanga.

    Kwa mujibu wa balozi Ramia, tathmini ni muhimu kufanyika kusaidia kujua athari zilizopatikana kipindi cha corona ambapo mambo mengi yamesitishwa kufanyika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako