• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam wa Kenya asema Marekani yaeneza habari zisizo za kweli kuhusu umaalum wa Taiwan

    (GMT+08:00) 2020-03-30 19:45:26

    Mtaalam wa uhusiano wa kimataifa wa Kenya anayefuatilia uhusiano kati ya China na Afrika, Cavince Adhere amesema, Marekani inaeneza hisia zisizo za kweli za upekee kwa Taiwan, na kutoa ishara mbaya kwa watu wanaotaka kujitenga kutaka uhuru wa Taiwan.

    Mtaalam huyo amesema, sheria ya mwaka 2019 inahusu Pendekezo la Ulinzi na Uboreshaji wa Wadau wa Kimataifa wa Taiwan, inatambua isivyo halali Taiwan kama sehemu halisi kisheria chini ya sheria na kanuni za kimataifa. Ameongeza kuwa kusaini muswada huo kuwa sheria ni ishara ya wazi ya Marekani kuiwekea shinikizo China, na kusema sheria hiyo inakwenda kinyume na uhusiano rasmi wa kidiplomasia ambao Marekani ilianzisha na China miaka 41 iliyopita.

    Licha ya hayo, amesema Marekani ilifahamu kuwa sheria hiyo inapingwa na China ikizingatiwa sera iliyopo ya China moja, ambayo imekubaliwa kama mfumo rasmi wa mawasiliano kati ya China na nchi nyingine.

    Amesema matokeo ya mvutano wowote kati ya Marekani na China pia yatahusisha sehemu zilizo nje ya mipaka ya nchi hiyo mbili kubwa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako