• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona yafikia 4,760 barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-30 19:57:07

    Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti magonjwa cha Afrika zimeonyesha kuwa, idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona katika bara hilo imefikia 4,760 kwa ujumla.

    Kituo hicho kimesema, Afrika Kusini, Misri, Algeria na Morocco ni nchi zenye hali mbaya zaidi barani Afrika. Viongozi wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wametoa wito wa kufanya ushirikiano wa kimataifa ili kupambana na virusi kwa pamoja, pia wamezitaka nchi zilizoendelea kuzipatia nchi za Afrika vifaa vya matibabu, vifaa vya upimaji pamoja na vifaa vya kukinga virusi.

    Kwa sasa, China inaendelea kuziunga mkono nchi za Afrika kwenye mapambano hayo. Vifaa vya matibabu vinavyotolewa na Mfuko wa Jack Ma na Mfuko wa Alibaba wa China vimeshapelekwa katika nchi za Mauritania, Senegal Gambia na Benin.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako