• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini asema hatua ya China ya kuweka vizuizi na kujitenga ni sahihi katika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-30 20:02:30

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema sera kali ya China ya kuweka vizuizi vya kutoka nje na kutokaribiana na watu zimeleta manufaa katika kuiweka nchi hiyo salama kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Rais Ramaphosa amesema hayo baada ya raia 114 wa nchi hiyo waliorejeshwa kutoka Wuhan, China, kuruhusiwa kwenda makwao jumapili baada ya kupimwa na kukutwa bila maambukizi ya virusi hivyo katika siku ya mwisho ya siku 14 walizowekwa karantini.

    Rais huyo amesema, ni kutokana na hatua kali zilizochukuliwa na serikali ya China ili kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo mjini Wuham, ndio raia hao waliweza kurejea nchini mwao wakiwa na afya na bila maambukizi.

    Rais Ramaphosa amesema, ni muhimu kuwa hatua ya kufunga nchi hiyo na hatua nyingine zote za dharura zinapaswa kufuatwa na kutekelezwa kwa wakati wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako