• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam wa Marekani asema virusi vya Vorona vimetoka kwa asili

    (GMT+08:00) 2020-03-30 20:08:14

    Mtaalam wa virusi kutoka Chuo Kikuu cha Tulane nchini Marekani Profesa Robert Garry hivi karibuni alipohojiwa na Shirika la habari la nchi hiyo ABC alisema, kwa mujibu wa uchambuzi wao, soko la vyakula vya bahari mjini Wuhan, China sio chimbuko la virusi vya Corona, kauli ambayo imefuatiliwa sana na jamii ta kimataifa.

    Tarehe 17, jarida la Nature Medicine lilitoa tasnifu iliyoandikwa kwa pamoja na wanayansi watano kutoka Marekani, Uingereza na Australia. Maoni makuu yaliyomo kwenye tasnifu hiyo yanasema, virusi vya corona "havikubuniwa katika maabara, wala sio virusi vinavyodhibitiwa na binadamu kwa malengo fulani". Tarehe 18, chuo kikuu cha Tulane katika tovuti yake kilitoa video ya mahojiano na mmoja wa waandishi wa tafsnifu hiyo ambaye ni mtaalam wa virusi kutoka chuo kikuu profesa Robert Garry. Katika video hivyo, Garry alisema, "naweza kukuambia kuwa virusi hivyo sio silaha ya kikemikali, wala havikutengeneza katika maabara, lakini vinatoka katika asili. Sasa hatujui virusi hivyo vimekuwepo miongoni mwa binadamu kwa muda gani, huenda ni miezi kadhaa, pia kuna uwezekano wa miaka hata miongo kadhaa, na baadaye vilibadilika na kuvifanya visambae kwa kasi kubwa."

    Tarehe 27, Shirika la habari la Marekani ABC lilimhoji Profesa Garry. Katika mahojiano hayo, profesa Garry alisema kinachopaswa kuzingatiwa ni kuwa, ingawa kuna watu wanahisi virusi vilitoka katika soko moja la vyakula vya bahari mjini Wuhan, China, lakini anaona hili ni kosa. "Kwa mujibu wa uchambuzi wetu na wa wanayansi wengine, virusi hivyo vilianza mapema kabla ya vile vilivyotokea katika soko hilo. Kule kweli kuna kesi za maambukizi, lakini sio chimbuko la virusi" Garry alisema.

    Hivi karibuni, kuna wanasayansi wengi wamegundua kwenye tafiti zao kuwa virusi vya Corona vinaweza kutokea mahali pengine.

    Tarehe 24, Januari, jarida la Lancet toleo la mtandao lilichapisha tasnifu iliyoandikwa na madaktari saba wa hospitali ya Jinyintan mjini Wuhan, ambao waliwafanyia utafiti wagonjwa 41 wa mwanzo, na kugundua kuwa 13 kati yao hawakuwahi kuwa karibu na soko la vyakula vya bahari la Huanan mjini Wuhan.

    Tarehe 26, Januari, jarida la Science lilichapisha makala iitwayo "pengine soko la vyakula vya baharini la Huanan mjini Wuhan sio chimbuko la virusi vipya vya Corona". Makala hiyo ilimnukuu mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza wa Chuo Kikuu cha Georgetown cha Marekani Profesa Daniel Lucey kuwa "watu hao 13 hawana uhusiano wowote na soko hilo, ni idadi kubwa sana." Anaona kuwa kama ni hivyo, pengine virusi vya Corona vinetoka mahali pengine.

    Naye mtaalam wa magonjwa ya kupumua wa China profesa Zhong Nanshan pia alisema maambukizi yalitokea kwanza China, lakini China sio chimbuko lake.

    Hivi karibuni, jopo la washauri bingwa la Canada Global Research lilitoa makala iliyoandikwa na Larry Romanoff ikinukuu uchambuzi uliofanywa na mtaalam wa virusi wa kisiwani Taiwan juu ya virusi vilivyotokea Iran na Italia, na kusema mipangilio ya vinasaba vya virusi iliyotangazwa na nchi hizo mbili ni tofauti na ule wa China. Makala hiyo pia inasema vyombo vya habari vya magharibi vinafuatilia kwa karibu China na kusababisha watu wengi kuona kuwa virusi vya Corona vinatokea China na kwenda nchi nyingine, lakini kwa hali ya sasa, hii imethibitishwa kuwa kosa.

    Tarehe 26, jarida la Cell lilitoa tahariri iliyoandikwa kwa pamoja na profesa Zhang Yongzhen kutoka kituo cha matibabu ya afya ya umma cha Chuo Kikuu cha Fudan, Shanghai, China na profesa Edward Holmes kutoka chuo kikuu cha Sydney, Australia. Tahariri hiyo inaona kuwa kabla ya mwezi Disemba mwaka 2019, huenda virusi vilikuwa vimebadilika katika maambukizi ya siri kati ya watu.

    Hivi sasa, nchi nyingi zimegundua wagonjwa ambao hawakutokea China. Kwa mfano, kuna mgonjwa jimboni California, Marekani hana historia ya kutembelea sehemu zilizoathiriwa vibaya na virusi vya Corona, wala hajawasiliana na mgonjwa anayethibitishwa; wagonjwa wawili wa kwanza nchini Iran nao pia hawajawahi kwenda China; nchini Japan kuna mwanamume mmoja alithibitishwa kuambukizwa virusi vya corona baada ya kurudi nchini humo akitokea Hawaii, na hakuenda China muda mfupi kabla ya kuambukizwa virusi.

    Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, mgonjwa wa kwanza anayejulikana nchini Uingereza aligunduliwa kuwa na virusi tarehe 31, Januari, lakini utafiti mpya umegundua kumekuwa na maambukizi ya virusi vya corona mapema katikati ya mwezi Januari, wao wanatoka familia moja katika kaunti ya East Sussex. Utafiti umegundua kuwa jamaa wa familia hiyo hawajawahi kuwa karibu na mchina mwezi mmoja kabla ya kuthibitishwa kuambukizwa virusi, lakini waliwasiliana na mmarekani.

    Je, virusi vinatokea wapi? Cha muhimu ni kuamini sayansi na kusikiliza maoni ya kitaaluma na kisayansi.

    Bila kujali virusi vinatoka wapi, ni kosa kuvihusisha na watu wa rangi fulani na wa nchi fulani, hayo ni maoni ya pamoja ya jamii ya kimataifa, pia ni maadili ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako