• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa vifaa vya kupambana na COVID-19 nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-07-03 10:07:55

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini Hua Ning na Shirika la utoaji wa misaada la Sudan Kusini chini ya usimamizi wa mke wa rais wa Sudan Kusini Bi. Mary Ayen Mayardit, waliendesha kwa pamoja hafla ya kukabidhi vifaa vya matibabu vya kupambana na COVID-19 vilivyotolewa na China kwa Sudan Kusini.

    Balozi Hua amesema, China na Sudan Kusini zinashirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona, na kwamba serikali na mashirika ya kiraia ya China yametoa awamu kadhaa za misaada ya kupambana na janga hilo nchini Sudan Kusini.

    Msaidizi wa Wizara ya Afya ya Sudan Kusini Mayen Machut Achiek ameishukuru serikali ya China kwa kutoa misaada hiyo, na kusema serikali ya China na watu wake wametoa misaada muhimu katika mapambano dhidi ya COVID-19 nchini Sudan Kusini, hatua ambayo imeonesha bayana urafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako