• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamiliki wa shule waonywa kuhusu ada

    (GMT+08:00) 2020-07-03 18:58:58

    Wizara ya Elimu na Mafunzo Zanzibar imewaagiza wamiliki wa shule binafsi wakiwamo walimu wakuu kutotoza ada ya masomo kwa wazazi kuanzia Aprili hadi Juni, mwaka huu.

    Agizo hilo linatokana na serikali kufunga shule zote kwa sababu ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.

    Hatua hiyo ya wizara imetolewa baada ya kubainika kuwa baadhi ya wamiliki wa shule hizo wamekuwa wakiwataka wazazi wa wanafunzi kulipa ada kwa kipindi ambacho wanafunzi hawakuwa shuleni jambo ambalo ni kinyume cha maagizo ya serikali.

    Waziri wa Wizara hiyo, Riziki Pembe Juma, amesema serikali iliamua kuzuia mikusanyiko ya watu na kusababisha masomo na shughuli zingine muhimu za kiuchumi na kijamii kusimamishwa.

    Pembe alisema wamiliki na walimu wakuu wote wa shule hawatakiwi kuwafukuza wanafunzi kwa kutolipa ada kwa kipindi serikali ilipofunga shule hizo.

    Alisema wazazi hawatoruhusika kulipia ada ya miezi iliyopita na badala yake walipe ada hizo kuanzia mwezi huu kwa mujibu wa sheria.

    Waziri alisema kumekuwa na mvutano baina ya wazazi na wamiliki wa shule binafsi juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa kipindi ambacho shule zilifungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako