• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sumukuvu yawapa hofu wakulima

    (GMT+08:00) 2020-07-03 19:03:50

    Wakulima wa mpunga katika Mkoa wa Morogoro wameiomba serikali kuwapa elimu zaidi juu ya uelewa wa sumukuvu. Hii ni baada ya wengi wao kuingiwa na hofu ya kuwepo kwa taarifa za vifo vinavyosababishwa na sumukuvu.

    Wadau wanasema wakulima wengi wana elimu duni inayotokana na uelewa mdogo wa sumukuvu, hali ambayo imekuwa ikichangia kuleta madhara kwa watumiaji wa vyakula vinavyotokana na kilimo.

    Wakulima hao walitoa ombi hilo wakati wakipatiwa mafunzo kuhusu madhara ya sumu kuvu na matumizi ya mbegu bora za kisasa yaliyotolewa na TARI Dakawa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na kuhudhuriwa na wakulima wa mpunga wa wilaya za Kilosa na Mvomero.

    Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Chakula, Josephine Amollo, amesema wizara imeamua kuanza kutoa elimu ya uelewa wa sumukuvu baada ya kubaini wakulima wa Mvomero na Kilosa licha ya kuzalisha mazao ya nafaka, lakini hawana mbinu za kuzuia uzalishaji wa sumukuvu kutokana na kukosa elimu.

    Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wakulima wa mazao ya nafaka wanaongeza uzalishaji wake kwa kutumia mbegu za teknolojia ya kisasa.

    Kwa upande wake, mkurugenzi wa Kituo cha TARI Dakawa, Dk. Andrew Ngereza, amesema wamezalisha aina tofauti za mbegu za mpunga ambazo zinauwezo wa kuhimili ukame na maeneo yenye maji ya chumvi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako