• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waraka wa China wa miaka 75 ya UM wathibitisha dhamira ya China ya kulinda utaratibu wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-09-11 18:41:38

    Wizara ya mambo ya nje ya China jana Alhamisi ilitoa Waraka wa Msimamo wa China kuhusu Miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, unaofafanua msimamo na maoni ya China juu ya hadhi ya Umoja wa Mataifa, hali ya kimataifa, maendeleo endelevu, ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona na masuala mengineyo.

    Wataalamu wanaona dunia ya leo inashuhudia mabadiliko makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika miaka 100 iliyopita, na janga la virusi vya Corona limeharakisha mabadiliko hayo na kuiingiza dunia katika kipindi cha machafuko. Lakini amani na maendeleo bado ni kaulimbiu ya zama za leo. China kutoa waraka huo wa msimamo katika mazingira hayo kumeonesha dhamira na imani ya China ya kushirikiana na nchi mbalimbali katika kuendeleza utaratibu wa pande nyingi, kusukuma mbele kwa pamoja maendeleo ya Umoja wa Mataifa, na kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

    Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa mambo ya Marekani iliyo chini ya Taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bw. Su Xiaohui, anaona waraka huo umesisitiza zaidi uhusiano kati ya China na dunia na uhusiano kati ya China na Umoja wa Mataifa, na kuonesha moyo wa uwajibikaji wa China.

    China ni moja ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Mataifa, na pia ni nchi ya kwanza iliyosaini Katiba ya Umoja wa Mataifa. Bw. Su Xiaohui amesema, katika miaka 75 iliyopita China imetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Umoja huo. China siku zote inajitahidi kuhimiza maendeleo endelevu, si kama tu itatimiza lengo la kutokomeza umaskini katika maeneo yote ya vijijini nchini China kama ilivyopangwa, na bali pia imefanya kadri iwezavyo kuanzisha majukwaa na kutoa fursa kwa ajili ya maendeleo ya pamoja ya pande mbalimbali, kupitia mapendekezo yake ikiwemo ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Mahusiano ya Kimataifa ya China Bi. Chen Fengying, anaona Umoja wa Mataifa umefanya kazi muhimu katika kulinda taratibu za pande nyingi, kusukuma mbele usimamizi wa dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Wakati dunia nzima inakabiliwa na janga la virusi vya Corona, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushikamana na kushirikiana kwa karibu zaidi. Amesema ni muhimu kwa China kutoa sauti yake kwa njia hii, na kuwafanya watu wote duniani kutambua umuhimu wa kulinda utaratibu wa pande nyingi, na kuendelea kuungana mkono katika kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako