• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa fedha wa China atoa mapendekezo matatu kuhusu kukabiliana na mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-18 17:14:39

    Mawaziri wa Fedha na Afya kutoka Kundi la Nchi 20 (G20) wamefanya mkutano kwa njia ya video kujadiliana kuhusu ukosefu wa kazi katika kukinga na kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 na mapedekezo ya kazi za baadaye.

    Waziri wa fedha wa China Bw. Liu Kun ameshiriki kwenye mkutano huo na kutoa mapendekezo matatu kuhusu jinsi ya kuboresha kazi ya kukinga na kukabiliana na janga la virusi duniani.

    Pendekezo la kwanza alilotoa waziri Liu ni kusukuma mbele operesheni ya pamoja. Amesema, China itaendelea kuunga mkono uongozaji wa Shirika la Afya Duniani katika kupambana na virusi. Pia amependekeza kuhimiza uwekezaji, na kwamba nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza ahadi ya kusaidia nchi zinazoendelea na kutoa misaada zaidi ya fedha kwao. Pendekezo la mwisho ni kuhimiza kuvumiliana na kushauriana, kuendelea kutekeleza mchakato wa huduma za afya kwa watu wote, kuongeza nguvu kulinda makundi yaliyo hatarini na kusukuma mbele kujenga jumuiya ya pamoja ya afya ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako