• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majaribio ya Chanjo ya COVID-19 ya Uingereza yaanzishwa tena nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2020-09-18 18:14:28

    Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza jana kimetangaza kuwa, mradi wa majaribio ya chanjo ya COVID-19 uliositishwa kutokana na kupata tathimini ya usalama, umeanza tena hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

    Chanjo hiyo iitwayo AZD1222 ilitengenezwa kwa ushirikiano kati ya taasisi ya Janner ya Chuo Kikuu cha Oxford na kikundi cha chanjo cha Oxford, na kampuni ya AstraZeneca ya Uingereza pia imeshiriki kwenye majaribio ya chanjo hiyo katika nchi mbalimbali duniani.

    Kutokana na mtu aliyepata chanjo hiyo nchini Uingereza kupata matatizo ya kiafya, chuo kikuu cha Oxford na kampuni ya AstraZeneca zilitangaza mapema ya mwezi huu kwamba, zitasimamisha majaribio yote ya chanjo hiyo.

    Tarehe 12 mwezi huu, chuo kikuu cha Oxford na kampuni ya AstraZeneca zimesema baada ya uchunguzi, usalama wa chanjo hiyo umeidhinishwa na kamati huru ya uchunguzi ya Uingereza na shirika la usimamizi, na inaweza kufanyiwa majaribio kwa binadamu.

    Professa Shabir Madhi wa chuo kikuu cha Witwatersrand cha Afrika Kusini amesema, shirika la usimamizi la Afrika Kusini na kamati ya maadili ya kitaaluma zinaona mradi huo wa majaribio ya chanjo unaweza kuendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako