• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia ateua waziri mkuu mpya

    (GMT+08:00) 2020-09-18 19:13:50

    Rais Mohamed Farmajo wa Somalia amemteua Mohamed Hussein Roble kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya Ali Hassan Khaire, ambaye aliondolewa na bunge mwezi Julai.

    Rais Farmajo, ametangaza uteuzi huo jana usiku, na kumwelekeza waziri mkuu mpya kuunda baraza jipya la mawaziri kuiongoza nchi hiyo kwenye kipindi cha mpito wakati Somalia ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu na mwaka ujao.

    Rais Farmajo amesema amemteua Roble kwa msingi wa uelewa wake, uzoefu na uwezo wake wa kutekeleza mapendekezo ya serikali, kuhimiza juhudi na kuendeleza mpango wa maendeleo wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako