• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Marekani yatishia kufunga shughuli za TikTok kwa hatua za kimabavu
    • Wanasiasa wa Marekani wanakwepa ushahidi wa mashambulizi ya kigaidi mkoani Xinjiang

    Mtandao wa Kimataifa wa Televisheni wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CGTN leo umetoa filamu inayoonesha hali halisi ya Mlima Tianshan: Kumbukumbu ya Mapambano dhidi ya Ugaidi mkoani Xinjiang.

    • Mapendekezo ya China yaelekeza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19

    Mapendekezo yaliyotolewa na rais Xi Jinping wa China katika mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika kuhusu ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 uliofanyika jana kwa njia ya video hayo yameelekeza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi vya Corona.

    • Sheria ya usalama wa taifa ni fursa ya kurejesha utulivu kwa Hong Kong

    • Uchumi wa China waendelea kufufuka

    Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika mwezi uliopita, viashiria vikuu vya uchumi wa China vimeboreka kwa mfululizo, na uchumi wa China umeendelea kufufuka.

    • Acheni kuichochea Afrika dhidi ya China

    Hivi karibuni baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi wamechochea tena uhasama kati ya China na Afrika. Mwanahabari wa Vision Group Mubarak Mugabo ametoa makala yenye kichwa cha Acheni kuichochea Afrika dhidi ya China.

    • Muungano wa Haki za Raia wa Marekani wasema ni wakati wa nchi hiyo kuacha kutumia vigezo viwili vya kibinadamu
    • Eneo la biashara huria la Hainan kuleta fursa mpya kwa maendeleo ya uchumi wa dunia

    Serikali ya China jana ilifanya mkutano na wanahabari, ikifafanua Mpango wake wa jumla wa Ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Hainan, na kutoa ishara kwamba, wakati mlipuko wa virusi vya Corona unafanya uchumi wa dunia udidimie, na vitendo vya kupinga mafungamano ya uchumi na kujilinda kibiashara vinaongezeka, China itaendelea kufungua mlango, na kushikilia utaratibu wa pande nyingi, ili kuhimiza mafungamano ya uchumi duniani.

    • Kutoa kipaumbele zaidi kwa watu ni uzoefu mkuu wa China katika kukabiliana na COVID-19

    Serikali ya China jana ilitoa waraka wa Kampeni ya China ya kukabiliana na COVID-19, ikirekodi mchakato mgumu uliopitiwa na watu wa China katika kupambana na ugonjwa huo, na kutoa uzoefu wenye ufanisi wa kukinga virusi na kutibu wagonjwa, na watu kupewa kipaumbele zaidi.

    • Marekani itapata hasara kubwa kama ikitengana na China

    Gazeti la the Wall Street Journal la Marekani hivi karibuni limetoa makala, ikiuliza kama Marekani iko tayari kupata hasara kubwa kwa kutengana na China. Makala hiyo inaonya kuwa wanasiasa wenye msimamo mkali dhidi ya China wanapaswa kutambua hasara kubwa zitakazotokea kutokana na Marekani na China kutengana katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara na elimu.

    • Marekani haina haki ya kutetea uhuru wa kutoa maoni kwa vitendo vyake vya kuwatendea vibaya wanahabari

    Maandamano makubwa kutokana na kuuawa kwa Mmarekani mweusi George Floyd na polisi mzungu yanaendelea nchini Marekani, huku wanahabari wengi wanaoripoti maandamano hayo wakitendewa vibaya na polisi. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Marekani haina haki ya kutetea uhuru wa kutoa maoni kutokana na vitendo vyake vya kimabavu dhidi ya wanahabari.

    • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ni tishio kweli kwa nchi za Ulaya

    Ingawa Marekani inakabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi, lakini waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo ambaye ni "waziri mbaya zaidi wa mambo ya nje wa Marekani katika historia" bado hajaacha kutoa kauli zisizo na msingi, akisema China inaharibu maslahi ya Marekani na wenzake wa Ulaya, ambao wanapaswa kushirikiana kupinga China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo ni tishio kwa nchi za Ulaya.

    • Marekani yachukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong

    Hivi karibuni mwanaume Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa jimbo la Minnesota, Marekani, aliuawa na polisi wazungu, na tukio hili limesababisha maandamano makubwa katika miji zaidi ya 70 nchini humo. Serikali ya Marekani imedai maandamano hayo ni vurugu, na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi ni wahalifu, na kuwasifu polisi waliogonga waandamanaji kwa gari na kusema ni mfano wa kuigwa. Pia imetishia kutuma majeshi na kuwafyatua risasi za moto waandamanaji. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema Marekani imechukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong.

    • Kudumisha utulivu wa uchumi wa China kusukuma mbele uchumi wa dunia

    Mkutano wa Bunge la Umma la China ulifungwa jana hapa Beijing. Kwenye mkutano na wanahabari baada ya kufungwa, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefafanua masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya uchumi wa China, kufungua mlango na ushirikiano, na kuonesha nia thabiti ya China katika kutimiza malengo ya maendeleo ya mwaka huu, kuboresha maisha ya watu na kuchangia maendeleo ya uchumi wa dunia.

    • Rais Xi asisitiza kutoa kipaumbele cha wananchi
    • China ina uwezo wa kutimiza malengo ya maendeleo

    Ripoti ya kazi za serikali inayotolewa kila mwaka kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China ni kiashiria muhimu cha mwelekeo wa maendeleo ya uchumi na utungaji wa sera. Ripoti ya mwaka huu haikutaja lengo la ukuaji wa uchumi, na imesisitiza kuhakikisha ajira na maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umaskini, na kujitahidi kumaliza ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anavuruga uhusiano kati ya China na Marekani

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitoa salamu za kumpongeza Tsai Ing-wen kwa kuapishwa kuwa kiongozi wa Taiwan, akimwita rais wa Taiwan, na kusema uhusiano kati ya Marekani na Taiwan ni wa kiwenzi. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo amekuwa kirusi cha kisiasa kinachovuruga uhusiano kati ya Marekani na China.

    • China ina uwezo wa kutimiza lengo la kutokomeza umaskini unaokithiri mwaka huu

    Mikutano miwili mikuu ya kisiasa nchini China ni majukwaa ya kutoa ishara za sera, na pia ni dirisha linalotumiwa na jamii ya kimataifa kutazama nchi hiyo. Katika mikutano hiyo ya mwaka huu, pande nyingi zinafuatilia jinsi China itakavyotimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii, haswa lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri.

    • Wanasiasa wa Marekani wanataka kuwa bingwa wa kukwepa wajibu?

    Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni kwenye mtandao wa kijamii ameweka barua aliyomwandikia mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus, akitishia kwamba, kama shirika hilo halitafanya mageuzi makubwa ndani ya siku 30, Marekani haitalifadhili tena, na kufikiria kujitoa kwenye shirika hilo. Kuhusu kauli hiyo, Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikiuliza, je, wanasiasa wa Marekani wanataka kuwa bingwa wa kukwepa wajibu.

    • Uchumi wa China wafufuka baada ya mlipuko wa COVID-19

    Mikutano Mikuu Miwili ya kisiasa nchini China itafanyika kuanzia kesho, wakati dunia inakabiliwa na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kudidimia kwa uchumi, jamii ya kimataifa inafuatilia sana jinsi China itakavyohimiza maendeleo ya uchumi wakati wa kukabiliana na virusi hivyo. Shirka Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema China ina imani na uwezo wa kushinda changamoto, na kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako