Wakulima watakiwa kuchukua mikopo ya pembejeo
2020-11-27 17:02:51| cri

Wakulima wa Mkoa wa Katavi nchini Tanzania wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha katika kuchukua mikopo ya pembejeo, ili kuwawezesha kufanya kilimo biashara na kukuza pato lao.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mpanda mkoani Katavi, Alex Massawe, wakati akifungua mkutano maalum na wakulima na wafanyabiashara wa mkoa huo.

Massawe alisema benki hiyo imekuwa ikikutana na wakulima wa maeneo tofauti kwa lengo la kutoa elimu ya kilimo biashara ambayo itamsaidia mkulima kuleta tija katika kilimo.

Akizungumzia mikopo ya pembejeo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa NMB, Wogofya Mfalamagoha, alisema benki inatoa mikopo ya pembejeo za aina tofauti kwa wakulima ambapo rejesho lake ni mara moja tu kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu.

Naye Mwakilishi wa NMB Foundation, Rogers Shipela, alithibitisha kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulim