China kupiga marufuku uagizaji wa taka zote ngumu kuanzia mwaka 2021
2020-11-27 20:32:17| CRI

Wizara ya Ikolojia na Mazingira, Wizara ya Biashara, na Idara ya Forodha zimetangaza kuwa China itapiga marufuku uingizaji wa taka ngumu kuanzia Januari 1, 2021.

Mamlaka hizo zimesema kutupa, kukusanya na kuziteketeza bidhaa taka kutoka nchi za nje kwenye eneo la China pia kutapigwa marufuku. Marufuku hiyo inatokana na sera iliyoanzishwa tangu mwaka 2017 ya kumaliza uingizaji wa taka ngumu, ambapo mwishoni mwa mwaka 2017 China ilipiga marufuku uingizaji wa aina 24 za taka ngumu, zikiwemo karatasi zisizopangwa, vitambaa na kemikali ya vanadium slag.

China ilianza kuagiza taka ngumu kama chanzo cha malighafi katika miaka ya 1980 na kwa miaka mingi imekuwa muagizaji mkubwa duniani. Lakini kutokana na uelewa wa watu kuhusu masuala ya mazingira na kichocheo kilichofanikiwa cha maendeleo yasiyo na uchafuzi ya China, uagizaji wa taka ngumu nchini sasa umepungua sana.