Sekta ya utalii Kenya yapata hasara ya shilingi bilioni 72
2020-11-27 17:02:24| cri

Ripoti ya serikali ya Kenya imesema sekta ya utalii nchini humo imepoteza jumla ya shilingi bilioni 72 kutokana na janga la corona. Waziri wa fedha wa Kenya Bw Ukur Yatani amesema sekta hiyo ambayo hutoa maelfu ya ajira imeathiriwa pakubwa na janga la corona huku hoteli za kulala pekee zikisemekana kupata hasara ya shilingi bilioni 56.  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya utalii na wanyama pori, hasara hiyo imetokana na kufungwa kwa safari za kimataifa pamoja na mipaka kutokana na janfa la corona. Ripoti hii inakuja wakati ambapo idadi ya watalii waliongia Kenya mwezi wa Aprili ilikuwa 3,101 ikilinganishwa na 146256 iliyoandikishwa kipindi kama hicho mwaka jana.Pia idadi ya wageni waliuotembelea mbuga za wanyama iliteremka kwa kiwango kikubwa na kufanya mapato kupungua kwa asilimia 90.