Wizara ya elimu ya China yazingatia kujenga uanaume kwa vijana wavulana
2021-02-02 20:49:12| cri

Kutokana na mswada uliowasilishwa na mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kuhusu kuzuia vijana wavulana kukosa uanaume na kuwa na tabia za kike, hivi karibuni wizara ya elimu ya China imesema, itaongeza walimu wa michezo shuleni, kurekebisha mfumo wa mafunzo ya michezo shuleni, na kuimarisha utafiti kuhusu elimu ya afya na hasa afya ya akili kwa vijana, ili kutatua vizuri suala hilo.

Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, Wizara ya Elimu ya China itautaka kila mkoa na kila shule, kuimarisha utekelezaji wa kanuni ya usimamizi wa walimu wa michezo, kuongeza nguvu katika kuinua uwezo wa walimu hao, kuboresha njia na mbinu za ufundishaji za walimu wa michezo, na kuzingatia zaidi kuwajengea uanaume wanafunzi wavulana.