SOKA: Chelsea yazamisha Atletico Madrid kwenye mzunguko wa kwanza wa UEFA
2021-02-24 16:01:33| cri

Bao la dakika ya 68 kutoka kwa fowadi wa zamani wa Arsenal, Olivier Giroud, 34, liliwapa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico Madrid ya Uhispania katika mzunguko wa kwanza hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) katika mechi iliyochezwa jana usiku. Mechi hiyo ilichezewa mjini Bucharest, Romania kutokana na ukali wa masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona. Ushindi huo wa Chelsea uliendeleza rekodi ya kutopigwa kwa kikosi hicho katika jumla ya mechi nane zilizopita chini ya kocha mpya Thomas Tuchel aliyeaminiwa kuwa mrithi wa Frank Lampard mnamo Januari 2021.