Guinea yaanza kutoa chanjo ya Ebola
2021-02-24 18:17:47| CRI

Guinea yaanza kutoa chanjo ya Ebola_fororder_VCG111318579575

Wizara ya afya ya Guinea jana imetangaza kuwa, nchi hiyo imeanza kutoa chanjo ya Ebola katika mji mkuu Conakry na eneo la Gbeke, kusini mashariki mwa jimbo la N'Zerekore.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema, mpaka sasa Jimbo la N'Zerekore limepokea dozi 3,500 za chanjo ya Ebola. Watu 11 waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa mjini Conakry wamepewa chanjo hiyo, na wengine 495 waliothibitishwa kuwa karibu na wagonjwa katika sehemu nyingine pia watapewa chanjo hiyo.