Kenya: Serikali za kaunti kenya Zapata idhini ya kukopa
2021-02-24 19:16:45| cri

Serikali za kaunti nchini Kenya zimepata idhini ya kukopa hadi shingingi bilioni 60 bilioni kwa miradi ya maendeleo katika makubaliano yaliyofikiwa kati ya baraza la Bajeti ya Serikali na wizara ya fehda.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Baraza la Magavana Ndiritu Muriithi amesema kaunti zinaweza kukopa hadi asilimia 20 ya mapato yao yaliyokaguliwa.

Kikomo cha juu cha shilingi bilioni 60 bilioni kinategemea mapato ya ukaguzi ya Mwaka wa Fedha 2018/19.

Awali, kaunti ziliweza kukopa pesa kutoka kwa benki kwa matumizi ya kawaida, lakini hakukuwa na kifungu cha kukopa kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu.