Viongozi wa Biashara wa EAC wataka uingizwaji wa DR Congo katika Jumuiya hiyo kuharakishwa
2021-02-25 19:46:33| cri

Sekta ya kibinafsi imewataka Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuelekeza vyombo vinavyohusika vya serikali kuharakisha ujumuishwaji wa nchi ya Kidemkrasi ya Kongo katika Jumuiya hiyo.

Hii ni moja ya vitu kwenye orodha ya matakwa ya Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) - kikundi cha vyama vya kibinafsi na mashirika - kabla ya Mkutano Mkuu wa kilele uliopangwa Jumamosi, Februari 27.

Rais wa Kongo Félix Tshisekedi mnamo Juni 8, 2019, alimwandikia Mwenyekiti wa EAC, Rais Paul Kagame wa Rwanda, akielezea hamu ya nchi yake kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo ya kikanda, ambayo sasa inaundwa na Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Sudan Kusini na Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa EABC ,Peter Mathuki, anasema kuwa DR Congo inatoa soko kubwa kwa biashara ndogo na za kati katika ukanda wa Afrika Mashariki.