SOKA: Barcelona yaifunga Elche 3-0 La Liga
2021-02-25 16:11:16| cri

Lionel Messi alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Barcelona kufunga Elche 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) jana usiku. Ushindi huo umekisaidia kikosi hicho cha kocha Ronald Koeman kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi wa msimamo wa Ligi hiyo Atletico Madrid hadi pointi tano pekee. Barcelona kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu kwa alama 50, mbili nyuma ya nambari mbili Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi. Hata hivyo, nafuu zaidi kwa Atletico, ni kwamba wana mchuano mmoja zaidi wa kutandaza ili kufikia idadi ya mechi ambazo tayari zimepigwa na washindani wao wakuu wakiwemo Real na Barcelona.