RIADHA: TOC yashangazwa aliyevunja rekodi ya taifa kutemwa Olimpiki
2021-02-25 16:09:11| cri

Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeeleza kushangazwa na Shirikisho la Riadha Tanzania kutomweka Augustino Sulle katika kikosi kitakachoshiriki mashindano ya Olimpiki. Sulle, mwanariadha mwenye kasi zaidi nchini Tanzania katika mbio za marathon, ni mmoja wa nyota ambao hawajawekwa kwenye timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya kutafuta viwango vya Olimpiki. Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, amesema wamepokea majina sita, lakini jina la Sulle halipo kwenye orodha hiyo. Sulle ana rekodi ya kukimbia kwa saa 2:07 katika mbio za marathon, rekodi aliyoiweka kwenye mbio za Toronto Marathon, Canada, msimu uliopita.