SOKA: 2021 AFCON U17: Tanzania yapangwa kundi B
2021-02-25 16:10:58| cri

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga makundi ya fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 Africa ‘2021 U-17 Cup of Nations’, zitakazounguruma nchini Morocco, baadae mwaka huu. Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyohusishwa kwenye upangaji huo wa makundi ikitokea ukanda wa Afrika Mashariki na kati sanjari na Uganda. Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepangwa Kundi B na timu za mataifa ya Nigeria, Algeria na Congo Brazaville. Hii ni mara ya pili kwa Serengeti boys kupangwa kundi moja na Nigeria, kwani waliwahi kupatwa na mtihani kama huo kwenye Fainali za 2019 zilizofanyika jijini Dar es salaam.