NDONDI: Miamba minne ya ndondi Tanzania vitani
2021-02-25 16:10:34| cri

Mashabiki wa ndondi nchini Tanzania watashuhudia miamba ya ndondi, Twaha ‘Kiduku’ Kassim, Abdallah Pazi, Francis Miyeyusho na Allan Kamote wakionyeshana umwamba kwenye masumbwi wikiendi hii. Mbabe atakuwa Dodoma kesho ijumaa kupambana na Daniel Wanyonyi, huku siku hiyohiyo, Twaha Kiduku atakuwa akipigana na Ulugbek Khakberdiev katika pambano litakaloitwa ‘Cairo Clash’nchini Misri, na Kamote atakuwa Tanga akizichapa na Jackson Malinyingi kwenye ukumbi wa Redoch. Mbali na mapambano hayo, bondia Francis Miyeyusho atakabiliana na Habibu Pengo katika ukumbi wa Next Door Arena, Masaki jijini Dar es Salaam.