Hali ya wakimbizi wa Eritrea katika eneo la Tigray bado ni ya wasiwasi
2021-02-26 09:18:23| CRI

Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR nchini Ethiopia Bibi Ann Encontre, amesema hali ya wakimbizi wa Eritrea katika jimbo la Tigray kaskazini mashariki mwa Ethiopia bado ni ya hatari, licha ya kuwa baadhi ya mambo yanaboreka.

Amesema kabla ya serikali ya Ethiopia kuanza kuchukua utekelezaji wa usimamizi wa sheria dhidi ya kundi la TPLF katika jimbo la Tigray, kulikuwa na wakimbizi laki moja wa Eritrea, kwenye maeneo ya kaskazini na kusini mwa jimbo la Tigray, lakini sasa UNHCR inaweza kufika kwenye kambi mbili za eneo la kusini, ambapo wamekuta wakimbizi elfu 30 tu.

Pia amesema licha ya kuwa serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa operesheni za kijeshi katika eneo hilo zimemalizika, mapambano ya hapa na pale yanaripotiwa mara kwa mara.