Kofia ya “mauaji ya kimbari” yafaa zaidi kwa baadhi ya nchi za magharibi
2021-02-26 09:40:36| CRI

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, baadhi ya nchi za magharibi zimeilaumu China kuhusu suala la Xinjiang kwenye mkutano wa 46 wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, madhumuni yao si kujali maslahi ya watu wa Xinjiang, bali ni kuingilia mambo ya ndani ya China na kuvuruga mchakato wa maendeleo ya China kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Bw. Zhao amesema nchi hizo hazipaswi kusahau historia yao ya kuwaua wakazi wa asili, na hata hivi sasa bado zinapuuza maslahi ya watu hao, kwa hiyo kofia ya “mauaji ya kimbari” inafaa zaidi kwa nchi hizo.

Ameeleza kuwa katika zaidi ya miaka 60 iliyopita, wastani wa urefu wa maisha mkoani Xinjiang umeongezeka kutoka miaka 30 hadi 72, na katika miaka 40 iliyopita idadi ya watu wa kabila la Wauyghur mkoani Xinjiang imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 100, na ongezeko la idadi ya Wauyghur ni mara 12 kuliko lile la watu wa kabila la Wahan kati ya mwaka 2010 na 2018.