Rais Macky Sall wa Senegal adungwa chanjo ya COVID-19 ya China
2021-02-26 09:41:10| CRI

 

 

Rais Macky Sall wa Senegal amedungwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Kampuni ya Dawa ya China, Sinopharm.

Wengine waliodungwa chanjo hiyo siku hiyo ni pamoja na baadhi ya maofisa wa serikali na wafanyakazi wa ofisi ya rais.

Baada ya kupewa chanjo hiyo, rais Sall amesema hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Senegal bado ni ya kutatanisha, na chanjo ni njia pekee ya kuzuia virusi hivyo.

Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ya Senegal zinaonesha kuwa hadi kufikia tarehe 25, watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo wamefikia 33,741, na kati yao 852 wamefariki. Serikali ya nchi hiyo imesema itajitahidi kuwapatia chanjo watu wote wanaotaka kabla ya mwaka 2022.