Balozi wa Nigeria asema uhusiano kati ya Nigeria na China ni kama ndoa
2021-02-26 10:29:12| CRI

 

 

Balozi wa Nigeria nchini China Baba Jidda Ahmad, amesema uhusiano kati ya China na Nigeria ni kama ndoa, na katika miaka 50 iliyopita tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi, ushirikiano wao umepata mafanikio ya kufurahisha.

Balozi Ahmad amesema katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China na Nigeria zimeimarisha ushirikiano unaonufaisha watu wao, na misaada iliyotolewa na China imeisaidia Nigeria kuongeza uwezo wa kujiendeleza.