Bandari ya Mombasa, Kenya yashuhudia ongezeko la mizigo baada ya zuio la COVID-19 kulegezwa
2021-02-26 09:06:49| CRI

Bandari ya Mombasa nchini Kenya imeshuhudia kuongezeka kwa mizigo inayoagizwa kutoka nje ya nchi, kufuatia kulegezwa kwa hatua na zuio la COVID-19 katika nchi kubwa duniani.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Kenya KPA Rashid Salim amesema kupitia taarifa kuwa bandari hiyo inatarajiwa kushughulikia makontena 115,000 mwaka huu, ikilinganishwa na 108,000 ya mwaka jana.