Kitendo cha kuingilia kati mambo ya ndani ya China chapingwa kwenye kikao cha UNHRC
2021-09-16 09:34:47| cri

Kitendo cha kuingilia kati mambo ya ndani ya China chapingwa kwenye kikao cha UNHRC_fororder_VCG111344966603

Nchi mbalimbali zikiwemo Tanzania na Sudan Kusini zimepongeza mafanikio ya China katika kulinda haki za binadamu huku zikipinga kitendo cha nchi za nje kuingilia kati masuala ya Xinjiang, Hong Kong na Tibet ambayo ni mambo ya ndani ya China.

Kwenye mazungumzo kati ya Kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UNHRC na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa OHCHR yaliyofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 15 mjini Geneva, mwakilishi wa Tanzania alitoa hotuba akisema, Tanzania inapinga kufanya suala la haki za binadamu kuwa la kisiasa, na suala la Xinjiang ni suala la ndani ya China na halitakiwi kuingiliwa na nchi za nje. Tanzania imepongeza juhudi za China katika kulinda na kuboresha maisha ya watu na pia mafanikio yake makubwa katika kuondoa umaskini uliokithiri, jambo ambalo ni mchango muhimu kwa shughuli za kupunguza umaskini duniani.

Mwakilishi wa Sudan Kusini kwenye hotuba yake alieleza kuunga mkono sera ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili” inayotekelezwa na serikali kuu ya China katika eneo la utawala maalum la Hong Kong, kufurahia haki za binadamu na uhuru walio nao wakazi wa Hong Kong, na kuipongeza China kwa kupitisha na kutekeleza sheria ya usalama wa taifa kuhusu Hong Kong.